
RAIS Samia Suluhu Hassan, leo Jumatatu ameanza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma Jumatatu ambayo ataihitimisha siku ya tarehe 28 mwezi huu.
Rais Samia akiwa mkoani humo atafanya mambo makubwa matatu ambayo ni kufunga tamasha la tatu la taifa la utamaduni linalomalizika leo na kufanya ziara ya kikazi kuanzia kesho tarehe 24 mpaka 28.

Alisema Rais atazitembelea wilaya tano za Mkoa wa Ruvuma ambapo ataongea na wananchi wa Mkoa huo kupitia mikutano ya hadhara na atazindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya mandeleo iliyoko mkoani humo.
RC alisema Rais Samia pia atashiriki mkutano wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa litakalofanyika wilayani Songea na atafunga kikao hicho tarehe 28 Septemba na kuhitimisha ziara yake siku hiyo ambayo pia ataongea na wananchi katika uwanja wa Maji Maji.

