×

Shambulio la Israel Lebanon Lasababisha Vifo 21 na Majeruhi 8

Takribani watu 21 wameuawa na wengine nane kujeruhiwa vibaya, katika shambulio la angani la Israel kaskazini mwa Lebanon

Shambulio hilo lilipiga jengo la makazi katika Aitou, kijiji chenye Wakristo wengi kilichokuwa mbali na maeneo ambapo Israeli imetekeleza mashambulizi dhidi ya Hezbollah, huku Israel haijatoa maelezo ya Moja Kwa moja kuhusiana na shambulio hilo.

Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa unasema kwamba walinda amani wake wataendelea kubaki Lebanon, licha ya madai ya mara kwa mara kutoka Israel kwamba wanapaswa kuondoka katika njia ya vikosi vyake .

Na kwingineko Washington Post inaripoti kwamba waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliiambia serikali ya Biden kwamba yuko tayari kuchagua hatua ya kupambana yenye mipaka zaidi kama jibu la shambulio la risasi la mwezi huu kutoka Iran.

Katika Gaza, Umoja wa Mataifa umeelezea kukerwa na idadi kubwa ya raia waliouawa kutokana na mashambulizi ya Israel kaskazini mwa eneo hilo katika siku za hivi karibuni.

Leave a Comment