
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amepokea tuzo nne za Kimataifa za World Travel Awards kwa mwaka 2024 ambazo Tanzania imezipata katika sekta ya Utalii huku akipongeza mchango wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuendeleza Sekta ya Utalii hapa nchini.
Akizungumza wakati wa kupokea tuzo hizo, Dkt Pindi amesema juhudi zilizofanywa na Dkt. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Dkt. Samia kupitia programu ya Tanzania-The Royal Tour na Amazing Tanzania zimeendelea kuing’arisha Tanzania katika sekta ya utalii kwa kupata Tuzo nne za kimataifa.

Amesema Dkt. Samia amekuwa mstari wa mbele kuleta mageuzi makubwa katika utangazaji utalii kupitia Programu ya Tanzania-The Royal Tour na Amazing Tanzania na kuwekeza katika kuboresha miundombinu ya utalii nchini.
Dkt. Pindi amesema juhudi hizo za Dkt. Samia zimechangia Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kunyakuwa tuzo nne za World Travel Awards kwa mwaka 2024.
Tuzo hizo ni Kivutio Bora cha Utalii Afrika (African Leading Tourism Attraction 2024) – Mlima Kilimanjaro na Hifadhi Bora ya Taifa Afrika (Africa’s Leading National Park 2024) – Hifadhi ya Taifa Serengeti.
Pia tuzo ya Kituo Bora cha Utalii Afrika (African’s Leading Destination)-Tanzania na Bodi Bora ya Utalii Afrika (African Leading Tourism Attraction 2024) – Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Dkt. Pindi amesema pia mawakala wa biashara za utalii wa hapa nchini nao wameshinda tuzo katika vipengele mbalimbali kutokana na juhudi zao za kutoa huduma bora katika sekta ya utalii.

Mawakala hao ni Gran Meliá Arusha, Twiga Tours, Lamai Serengeti, Kuro Tarangire, Altezza Travel, Satguru Travel Tanzania, Skylink Travel & Tours na Gosheni Safaris.
“Niwapongeze mawakala hawa kwa tuzo walizopata kutokana na kazi nzuri waliyoifanya katika sekta ya utalii.”
Dkt. Pindi pia ameipongeza Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kwa kufanikisha Visiwa vya Zanzibar kushinda tuzo ya eneo maridhawa kwa Matukio na Matamasha.
Aidha, amesema faida za Tanzania kushinda tuzo hizo ni kuwa zitasaidia kuendelea kuvutia watalii, kuongeza mapato

