
ALIYEKUWA Waziri wa Usalama wa ndani nchini Kenya, Profesa Kithure Kindiki leo Novemba 1, 2024 ameapishwa rasmi kuwa naibu rais mpya wa Kenya.
Kithure Kindiki anachukua mahala pake Rigathi Gachagua aliyeondolewa madarakani.
Kindiki anachukuwa wadhfa huo baada ya siku kadhaa za makabiliano ya mahakamani kati ya mawakili wa aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua na wale wa serikali.
Gachagua alikwenda mahakamani kuzuia kuapishwa kwa Kindiki baada ya kudai kwamba aliondolewa madarakani kinyume na sheria.
Hafla ya kuapishwa imefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi.