
Mmoja wa nyota walioshiriki katika filamu maarufu Hollywood ya “The Hitman’s Bodyguard” Ori Preffer (Vacklin) na mkewe ambaye pia ni mwanamitindo na mtangazaji mashuhuri nchini Israel, Yael Goldman, wamemaliza ziara ya kutalii hapa nchini katika Hifadhi za Ngorongoro, Serengeti na kwenda visiwani Zanzibar.
Akionekana kufurahia vivutio vya Tanzania, nyota huyo aliyeshiriki pia filamu ya mtayarishaji mkubwa duniani Mel Gibson (known for The Passion of Christ) ya “Hacksaw Ridge“ akiwa na mkewe na wanafamilia yao amepost picha nyingi lakini akiandika kwa Kiswahili “Tanzania Yetu Hakuna Matata.”
Bila shaka nukuu yake hiyo ya “Hakuna Matata” imetosha kuwafikishia ujumbe nyota na mastaa wengine mbalimbali na mashabiki zake kote duniani kuwa kama kuna mahali wanapaswa kwenda kuvinjari na hakuna shari basi ni mbugani na katika vivutio vingine nchini Tanzania.

