
Waziri wa Viwanda Biashara na Viwanda Mhe. Dkt. Seleman Jafo azindua rasmi Gulio la kwanza la biadhaa za ushonaji, Usindikaji na ushonaji Mkoani Lindi ulioenda sambamba na uzinduzi wa mfumo wa uuzaji wa bidhaa Mtandaoni uliopewa jina ya Lindi katika Uchumi wa Viwanda -E Soko (LIKUVI ) ambao utahusisha utangazaji na uuzaji wa bidhaa mtandaoni.
“Nimefurahia sana mfumo wa uuzaji wa bidhaa mtandaoni E- Soko, biashara za hapa nyingi zitakwenda kimtandao na wafanyabiashara wataweza kuuza zaidi . Ninyi mmekuwa Mkoa wa kwanza wa mfano kwa jambo ili , wengine wote watakuwa (copy and paste) wataiga kutoka mkoa wa Lindi. ” Mhe. Seleman Jafo.
Mhe Jafo, ameyaeleza hayo akizindua Gulio hilo la kwanza ambalo limekutanisha wajasiriamali zaidi ya Mia nne kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi na nje ya Mkoa wa Lindi

Aidha, Mhe. Dkt. Jafo amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack na viongozi wa Mkoa huo kwa ubunifu wao wa kuandaa tukio kubwa linalo wakutanisha wajasiriamali kutoka halmashauri zote za Mkoa wa Lindi na nje ya Mkoa wa Lindi .
“Nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwa kuanda tukio kubwa ambalo linawakutanisha wafanyabiashara wadogo na kupata fursa ya kuuza biashara zao nakuongeza wigo wa maarifa” Mhe. Dkt Jafo.
Ametumia fursa hiyo kuwasisitiza viongozi wa halmashuri kuendelea kutoa mikopo ya asilimia kumi kuwezesha vikundi vya wajasirimali wenye viwanda vidogo vidogo kufikia malengo yao wakati mpango na utaratibu wa kuendelea kujenga na kufufua viwanda vya Mkoa wa Lindi ukiendelea.

kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. zainab Telack amemshukuru Waziri wa viwanda kwa kuitikia wito na kueleza namna mkoa wa lindi ulivyojikita katika uzalishaji wa mwani na zao la ufuta hivyo uwepo wa viwanda wa kuchakata na kusindika mazao hayo ni muhimu sana kwa Mkoa wa Lindi.
Mratibu wa Gulio hilo ambaye ni Mkuu wa diveshini ya Viwanda, biashara na Viwanda ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dkt. Bora Haule amesema gulio hilo litakuwa endelevu ambalo litafanyika mara mbili kila mwezi lengo kuwatafutia Masoko na kuwaongezea wigo wa maarifa zaidi.
