×

Makamu wa Rais Azungumza Baada ya Kuwasili Baku nchini Azerbaijan 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango azungumza na Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakaoshiriki Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) mara baada ya kuwasili Baku nchini Azerbaijan  Novemba 9, 2024.

Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 11 – 22 Novemba 2024 Jijini Baku.

ALIYEZIMIA MBELE ya JENEZA LA TESSA wa HUBA AFUNGUKA KWA MARA ya KWANZA – AFICHUA KILICHOMPATA…

Leave a Comment