
Dar es Salaam, 22 Novemba 2024: Uongozi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kilichopo Mlimani jijini leo umeungana na Taasisi ya Empower Limited katika uzinduzi wa mpango maalum unaolenga kuandaa viongozi watakaosimamia safari ya Tanzania kuelekea maono ya 2050, ambapo mpango huu wa uongozi umelenga kuwapa mameneja wa kati na waandamizi pamoja na wasimamizi ujuzi muhimu wa kuleta maendeleo, kuhamasisha ubunifu na kuiongoza Tanzania katika mustakabali mzuri zaidi.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar-es-Salaam kwenye uzinduzi huo, Mwenyekiti mshirika wa Empower Limited, Miranda Naiman, amesema kuwa ushirikiano huo umewawezesha kachanganya maendeleo ya uongozi wa kivitendo na ubora wa kitaaluma.
“Visionary Leaders Programme inawataka viongozi wa kizazi kijacho kuelekeza Tanzania katika maono ya 2050, ikilenga ukuaji endelevu na ubunifu Katika kila ngazi” amesema Naiman.
Nae Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utafiti wa UDSM Prof. Nelson M.K. Boniface, amesema kuwa ushirikiano huo unaonyesha dhamira ya UDSM ya kukuza viongozi watakaoweza kusimamia mustakabali wa Tanzania kupitia mpango huo, watawapa wataalamu ujuzi na maarifa yanayohitajika na changamoto za kiuchumi na kijamii za nchi yetu. Alimaliza kusema.