×

Kapinga: Sekta Binafsi Ni Nguzo Muhimu ya Maendeleo ya Taifa

Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Judidh Kapinga akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa Chapa mpya ya Magari ya Jetour nchini Tanzania,iliofanyika Juni 8,2026 Masaki, jijini Dar es Salaam

Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amesema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara ili kuvutia uwekezaji wenye tija. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chapa ya magari Jetour jijini Dar es Salaam, alisema uwekezaji huo unaunga mkono Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na ajenda ya uchumi wa viwanda.

Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Tanzania Mhe. Andrey Avetisyuan akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa Chapa mpya ya Magari ya Jetour nchini Tanzania.

Alieleza kuwa ushirikiano kati ya Africarriers Group na Jetour utachochea biashara, uwekezaji, uhamishaji wa teknolojia na ajira kwa Watanzania. Aidha, aliipongeza Africarriers kwa mchango wake wa zaidi ya miaka 50 na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji wanaochangia maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Sheria wa Kampuni za Africarriers, Ngasa Mboje, alisema magari ya Jetour yameletwa kwa kuzingatia mahitaji ya soko la Tanzania na yanapatikana kwa malipo ya moja kwa moja au kwa mkopo ili kuwapa Watanzania wengi zaidi fursa ya kuyamiliki.

Makamu wa Rais wa Kampuni ya Magari ya Africarriers Group,Bw. Shahid Nabi, akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa Chapa mpya ya Magari ya Jetour nchini Tanzania
Baadhi ya Viongozi na wageni waalikwa wakishuhudia uzinduzi wa Chapa mpya ya Magari ya Jetour nchini Tanzania
Mwenyekiti wa Makampuni ya Africarriers, Bw. Fida Rashid, akimkabidhi Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian mfano wa gari ya Jetour iliozinduliwa nchin Tanzania.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian akiwasha gari ya Jetour iliozinduliwa nchini Tanzania hapo jana,Masaki jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Chapa mpya ya Magari ya Jetour nchini Tanzania,hafla iliofanyika Juni 8,2026 Masaki, jijini Dar es Salaam.

Leave a Comment