
RAIS wa Marekani Joe Biden ametoa msamaha rasmi kwa mtoto wake Hunter, ambaye alikuwa anakabiliwa na kesi mbili za uhalifu, licha ya kwamba awali, alikuwa ameondoa uwezekano wa hilo.
Hunter Biden alikiri mashtaka ya kukwepa kulipa ushuru mapema Septemba, na alipatikana na hatia ya kuwa mtumiaji haramu wa dawa za kulevya na kumiliki bunduki mnamo mwezi Juni – na kuwa mtoto wa kwanza wa rais aliyeko madarakani kuhukumiwa kwa uhalifu.
Msamaha kamili usio na masharti wa Joe Biden kwa mtoto wake unawadia baada ya rais kusema hapo awali kuwa hatatoa msamaha kwa mtoto wake.
Lakini Jumapili jioni, Rais Biden alisema ingawa anaamini katika mfumo wa haki, “siasa zimeingia katika mchakato huu na kusababisha kukosekana kwa haki”.