×

Ikulu ya Marekani Yatetea Msamaha wa Biden kwa Mwanawe

Ikulu ya White House imetetea msamaha wa Rais Joe Biden kwa mtoto wake, Hunter, baada ya kusisitiza mara kwa mara kwamba hana mpango wa kutoa huruma kama hiyo.

Waziri wa habari Karine Jean Pierre alisema Biden amemsamehe mtoto wake wa kiume, ambaye alikuwa akikabiliwa na hukumu baadaye mwezi huu katika kesi mbili, ili kumkinga dhidi ya mateso yanayoweza kutokea kutoka kwa maadui wa kisiasa wa rais anayeondoka.

Msamaha huo wa wigo mpana unahusu uhalifu wowote ambao Hunter mwenye umri wa miaka 54 anaweza kuwa alifanya katika kipindi cha muongo mmoja.

Warepublican wameshutumu hatua hiyo, huku rais mteule Donald Trump akiutaja kuwa unyanyasaji na upotovu wa haki.

Rais wa chama cha Democratic alitoa msamaha huo Jumapili jioni kabla ya kuanza safari rasmi kuelekea barani Afrika.

Bi Jean Pierre alizungumza na waandishi wa habari: “Anaamini katika mfumo wa haki, lakini pia anaamini kwamba siasa mbaya ziliathiri mchakato huo na kusababisha kukosekana kwa haki.”

PASTOR PHIILIPO AFUNGUKA MAZITO – ”SIO KILA IMANI ni YA KUKIMBILIA – KUNA VITU VINGI VINAENDELEA”

Leave a Comment