
Mwenyekiti wa Ngome ya vijana wa, Abdul Nondo anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam kutokana na kuumizwa kwa kupigwa na watu wasiojulikana.
Ikumbukwe kuwa Desemba 1, 2024 Abdul Nondo alidaiwa kutekwa asubuhi akiwa kituo cha mabasi cha Magufuli Mbezi Louis jijini Dar es Salaam na watu wasiojulikana akitokea mkoani Kigoma alikokuwa sehemu ya viongozi wa Kitaifa walioongoza kampeni kwenye mikoa ya Magharibi mwa Tanzania.
Na taarifa iliyotolewa jana Desemba 2, 2024 na Msemaji wa Jeshi la Polisi DCP David Misime ilisema, Nondo alieleza kuwa alitelekezwa maeneo ya fukwe za Coco (Coco beach) Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu asiowafahamu.
Pia taarifa hiyo, inaeleza kuwa baada ya kutelekekezwa alisimamisha bodaboda na kumwelekeza amfikishe katika Ofisi za Chama chake zilizopo Magomeni jijini Dar es Salaam ambapo walifika muda wa saa tano usiku, ambapo alionana na Viongozi wake na kupelekwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.



PASTOR PHIILIPO AFUNGUKA MAZITO – ”SIO KILA IMANI ni YA KUKIMBILIA – KUNA VITU VINGI VINAENDELEA”