×

Kocha wa Man United Kuiongoza timu yake Dhidi ya Arsenal leo

Kocha wa Manchester United Ruben Amorim (39), baada ya kuiongoza timu yake kupata ushindi mnono Jumapili iliyopita dhidi ya Everton, leo atakuwa na kibarua kizito mbele ya Arsenal ya Mikel Arteta katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza pale Emirates majira ya saa 5:15 usiku.

Manchester United imeonekana kuimarika chini ya Mreno Ruben Amorim, Jumapili iliyopita ilipata ushindi wa mabao 4-0, wakati mpinzani wake wa leo Arsenal alipata ushindi wa mabao 2-5 dhidi ya West Ham, ambayo jana imekumbana na kichapo kutoka kwa mbweha Leicester City.

Arsenal iko nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza ikiwa na alama 25, wakitofautina na Manchester United alama 6, huku Man United akiwa na alama 19 katika nafasi ya 9.

Arsenal inapambana kupunguza tofauti ya alama dhidi ya vinara Liverpool, ambapo mpaka sasa tofauti yao ni alama 9, wakati Manchester United inapambana kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hiyo.

MZEE WARIOBA ATEMA NYONGO KILICHOTOKEA UCHAGUZI wa SERIKALI za MITAA – UHUSIKA wa POLISI…

Leave a Comment