Mshereheshaji na mchekeshaji ambaye pia ni mtumishi wa Mungu, Mc Pilipili amefunguka kupitia Global TV katika kipindi cha Kontena na kueleza kuwa ameshawahi kufanya kazi ya U-MC mpaka nchini Marekani.
Mc Pilipili amesema kwamba katika sherehe ambazo yeye huwa mshereheshaji hasa mikoani, watu huwa wananunua kadi hata za harusi zisizowahusu ili waingie na kumuona kutokana na jinsi anavyowaburudisha.