×

Watu 14 Wafariki na Wengine 8 Kujeruhiwa katika ajali Mikese, Morogoro – Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima akiongea baada ya kufika hospital ya Rufaa Mkoa Morogoro.

Watu 14 wamefariki Dunia na wengine 8 kujeruhiwa katika ajali iyohusisha Lori la Mizigo lililokuwa linatokea Dar kwenda Morogogoro na Coaster iliyokuwa inatokea Morogoro kwenda Dar usiku wa kuamkia leo eneo la Mikese barabara kuu ya Morogoro -Dar es Salam.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mkoa Morogoro Nkungu Daniel amethibitisha kupokea kwa miili hiyo na majeruhi ambapo amesema waliofariki bado miili yao haijatambulika.

Nkungu amesema kati ya marehemu 14 wanaume ni 8 na wanawake 6 huku majeruhi wanaendelea na Matibabu katika hospitali hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima amefika hospital ya Rufaa Mkoa Morogoro wanakopatiwa matibabu majeruhi hao ambapo ametoa wito wananchi kufikia katika hospital hiyo Ili kutambua miili ya ndugu zao.

Katika ajali hiyo madereva wote wamepoteza maisha.

Leave a Comment