×

Lipumba Aibuka Kidedea Uchaguzi Mkuu CAF

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa Prof. Ibrahim Lipumba

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa Prof. Ibrahim Lipumba ametetea tena nafasi yake baada ya kuibuka kidedea kwa mara nyingine tena katika uchaguzi mkuu uliofanyika Desemba 18.2024 ambapo Prof. Lipumba amepata kura 216 ya kura zote

Kura zote zilizopigwa zilikuwa ni 596, kati ya hizo kura halali 592 na kura nne (4) ziliharibika

Katika uchaguzi huo uliokuwa na wagombea tisa (9) wagombea wengine walikuwa ni Ali Juma Khamis ambaye alijitoa ‘dakika za mwisho’, mgombea wa pili alikuwa ni Athman Kanali aliyepata kura tano (5), Hamadi Hamadi alipata kura 181, Juma Shaban alipata kura sita (6), Maftaha Abdallah Nachuma alipata kura 102, Wilfred Lwakatare amepata kura 78, Ngaitile Siwale amepata kura mbili (2) na Chifu Lutalosa Yemba amepata kura mbili (2)

“Kwa matokeo haya niliyonayo na kwa nafasi yangu ya Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi namtangaza Ibrahim Lipumba kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa uchaguzi wa chama cha wananchi (CUF), ndugu zangu kwa mgombea yeyote yule ambaye kwa namna yoyote ile hajaridhika na matokeo haya nilipoanza asubuhi nilisema kuwa tunayo kamati ya rufani ya uchaguzi Taifa, na kamati hii inatakiwa ifanye kabla mkutano mkuu huu haujakamilika, yeyote ambaye hajaridhika iwe kwa matokeo au kwa tafsiri ya kikanuni au kisheria anakaribishwa kuwasilisha rufaa yake kwa kamati ya uchaguzi siku ya kesho (leo, Alhamisi Desemba 19.2024) wakati sisi tunaendelea na uchaguzi wa nafasi nyingine” -Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi CUF Taifa

LISSU AKASIRIKA KUAMBIWA ATASHINDWA UCHAGUZI – ”KWANINI MNAFIKIRI MBOWE LAZIMA ATASHINDA?”…

Leave a Comment