×

TGNP Yaendesha Kongamano la Wanawake na Uongozi Jijini Dar es Salaam

Mtandao wa Jinsia nchini (TGNP) imefanya Kongamano la wanawake na Uongozi Leo Desemba 18,2024, jijini Dar-es-Salaam ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘tutafakari na maono kuelekea miaka 30, ya Beijing na Dira 2050’

Akizungumza wakati wa kongamano hilo, Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi amesema wanayo furaha kuona uchaguzi wa serikali za mitaa namna wanawake wengi wameitikia na kushika nafasi za wenyeviti naamini nafasi za wanawake dmzitaendelea kuongezeka.
kwenye uchaguzi wa 2019 ni madiwani, na kwamba asilimia 2.1 ya wanawake wali

“Tunayo imani kwamba kuna uchaguzi wa mwaka ujao data zitakuwa tofauti lakini hapa tunayo mifano ya wanawake waliopasua miamba kwenye uchaguzi uliopita,”amesema Liundi.

Mmoja wa wanaharakati ambaye alikwenda Beijing kwa ajili ya kupigania haki za wanawake Bi.Zakia Meghji amesema kuwa baada ya miaka 30 hali imekuwa tofauti Katika sekta mbalimbali na kuona wanawake nao wanapewa nafasi.

“Tulikwenda Beijing na wakati ule nilikuwa Waziri wa Afya,ndio niliongoza kikosi cha uwakilishi upande wa Serikali na tulieleza maswala mbalimbali ambayo tunataka mabadiliko mojawapo ilikuwa swala zima la Elimu,uwakilishi wa wabunge ndani ya Bunge,na maswala ya Afya.

“Hivyo Katika miaka 30,tunakuta kwamba japokuwa siyo kubwa sana mfano mwaka 1985 nilipokuwa mbunge wa viti maalumu,mle bungeni kulikuwa na mbunge wa Jimbo mmoja tu ambaye ni Shamim Khan, lakini Sasa hivi,wamepata moyo zaidi wa kugombea na wale wanaowachagua huko vijijini wanakuwa wanawaamini wanawake ndio maana Kuna wabunge wengi ukilinganisha na miaka ya nyuma.

“Naomba niwashukuru wote ambao nilikuwa nao katika mapambano sifa ziende kwao wote siyo kwangu tu kwa maana jitihada zile ndio zimefanikisha haya mpaka Sasa mwanamke anaaminiwa kwenye uongozi,” amesema Meghji.

Nae Bi Getrude Mongela amesema kuwa anatambua TGNP kwa sababu alipoteuliwa kuwa Katibu mkuu alipata nafasi ya kurudi Tanzania, na kukaribishwa katika Mkutano wao, wakapeana mioyo na akawaomba wazunguke nchi nzima, ili kuelezea kuhusu mkutano wa Beijing na ufahamike.

” Nyie huwa mnandaliwa mwenzenu nilienda kuandaa mwenyewe Mkutano na kilichonisukuma siku hiyo nilikuwa balozi India, mara nikapata simu kutoka kwa mwanamke Mmoja aliyekuwa ananifahamu Australia, akaniambia kuwa safari hii kutakuwa na na Mkutano Beijing na safari hii ni zamu ya Afrika kutoa katibu mkuu kwa hiyo nakuomba uombe,nikaogopa kwa sababu nimepewa ubalozi wa India and hata miaka miwili bado naanzaje kumwambia RAIS,nikapata simu nyingine tena kutoka kwa rafiki yangu kutoka Ghana,akaniambia naomba uombe nafasi hiyo,

“Nikawa na mawazo hadi watoto wangu wakaniuliza mbona siku hizi umekuwa mtu wa mawazo? Nikawaambja napokea simu nyingi waliniambia niombe nafasi Katika umoja wa Mataifa lakini naona haya kwenda kumwambia RAIS sijakaa hata miaka miwili kwenye nafasi aliyonichagua,ndipo mtoto wangu Mmoja akaniambia umesoma Biblia?

“Nikamwambia nimesoma akaniambia tena umesoma vile vipengele vya hadidhi za watu waliogaiwa talatla,? Nikamjibu ndio nimesoma akasema basi una kitu ndani yako ndio maana unapigiwa simu,
hivyo nikaandika barua na kupeleka na hatimaye nikachaguliwa na hapo ndio safari yangu ilipoanzia na hatimae matunda tunayaona ingawa siyo kwa ukubwa huo, naamini itaendelea kuimarika zaidi.

“Uchaguzi mkuu tuwatafute wagombea wanawake sahihi si tu kwa sababu ni mwanamke tuwape moyo ili mwaka kesho tupate hiyo asilimia kubwa tunayoitaka,” amesema Bi Mongella.

Leave a Comment