×

Watu 5 Wafariki Dunia Kwa Kupigwa na Radi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linapenda kutoa taarifa kuhusu matukio mawili muhimu yaliyotokea katika Mkoa wa Mbeya, yakiwemo tukio la vifo vya watu watano wa familia moja huko Wilaya ya Chunya na tukio la wizi wa mtoto Wilayani Mbarali.

Mnamo tarehe 29 Desemba 2024, majira ya saa 8:30 usiku, katika Kitongoji cha Nkangi, Kijiji cha Isangawana, Kata ya Matwiga, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, watu watano wa familia moja walifariki dunia baada ya kupigwa na radi wakati wakiwa wamelala kwenye kambi ya kuchungia ng’ombe. Waliopoteza maisha katika tukio hili ni: Balaa Scania (28), Kulwa Luweja (17), Masele Masiganya (16), Hema Tati (10), Manangu Ngwisu (18)

Aidha, watu watano walijeruhiwa katika tukio hilo. Majeruhi hao ni: Gulu Scania (30), Manyenge Masaganya (13), Seni Solo (13), Paskali Kalezi (16), Huzuni Kalezi (19)

Majeruhi walikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Isangawana ambapo walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani baada ya hali zao kuimarika. Tukio hili lilisababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku huo, ikiambatana na radi.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua kwa kuepuka maeneo hatarishi, hususan kukaa karibu na miti mikubwa.

Leave a Comment