×

TRA Yavunja Rekodi ya Makusanyo Tangu Kuanzishwa Kwake


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imerekodi ongezeko la asilimia 17.6 ya makusanyo yake ya Desemba 2024 ikilinganishwa na Desemba 2023.

Hayo yamebainishwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda akisoma taarifa ya makusanyo ya kodi kwa kipindi cha Julai hadi Desemba, mwaka wa fedha 2024/2025 leo Jumatano Januari 1, 2025 jijini Dar es Salaam.

“Mamlaka ya Mapato Tanzania imevunja rekodi ya makusanyo tangu kuanzishwa kwake kwa kukusanya Sh3.587 trilioni kwa Desemba sawa na asilimia 103.52 ya lengo ambalo lilikuwa ni kukusanya Sh3.465 trilioni ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 17.59 ukilinganisha na kiasi cha Sh3.05 trilioni zilizokusanywa Desemba 2023,”amesema Mwenda.

MSUMENO wa KAMANDA WAONDOKA na DEREVA BAJAJI – BODABODA MATATANI……

Leave a Comment