
Mwanachama maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bob Chacha Wangwe amesema ameamua kumuunga mkono Tundu Lissu badala ya Freeman Mbowe katika kuwania uwenyekiti wa chama hicho Taifa kutokana na mahitaji ya kisiasa nchini ambayo anaamini mtu sahihi wa kukikomboa chama chake kwa sasa ni Lissu
Akihojiwa na wanahabari Januari 3, 2025 Bob ambaye pia ni wakili amesema katika nyakati hizi ambazo mazingira ya siasa na demokrasia ya Tanzania imeminywa kwa kiasi kikubwa hadi kufikia hatua ya kile alichodai uporaji wa chaguzi mbalimbali za Kitaifa.
“Tuhuma za rushwa ndani ya chama chao, utekaji na mauaji hasa kwa wafuasi wa chama hicho nk, ni wazi kuwa Chadema inahitaji mtu mwenye ushawishi anayeweza kusimama kidete dhidi ya nguvu ya watawala na kuongoza harakati za mageuzi ya kweli na mtu huyo ni Lissu.” Anasema Wangwe.
“Natambua kazi kubwa iliyofanywa na Freeman Mbowe katika kipindi chote cha takribani miaka 21 aliyoongoza Chadema kama Mwenyekiti wa Taifa, lakini yeye mwenyewe (Mbowe) ni vyema angetumia busara zake kutowania nafasi hiyo tena ili kutoa nafasi kwa Tundu Lissu, Anasema Lissu.
Kwa mujibu wa Bob Wangwe anaamini kwamba ni turufu nzuri kwa chama hicho kuelekea kwenye mageuzi wanayoyapigia kelele kwa muda mrefu kumchagua Lissu kuongoza Chadema.