
Maafisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) kutoka Los Angeles, kwa mara nyingine wamevamia nyumbani kwa staa mkubwa wa filamu Hollywood na mtalaka wa mwanadada Jennifer Lopez (j-Lo), Ben Affleck zikiwa ni siku mbili tu tangu walipovamia tena Jumapili iliyopita.
Video na picha zimewaonesha maafisa hao wakiwa wamepaki gari lao kuliziba geti la Ben Affleck kabla ya baadaye kuonekana wakiwa ‘wanakoromeana’ na Ben Afleck ambaye alitoka akiwa ndani ya gari na kukuta wameziba geti lake.
Inaelezwa kuwa, sababu ya maafisa hao wa FBI kumfuatilia Ben, ni kutokana na tukio la ‘drone’ binafsi kugongana na ndege ya kuzima moto unaoendelea kuwaka Los Angeles na kusababisha maafa.
‘Drone’ hiyo inadhaniwa kuwa ya Ben Afleck ingawa bado ushahidi wa kutosha haujapatikana.
Tangu kuzuka kwa moto, Ben Afleck ni miongoni mwa mastaa wanaopamba vichwa vya habari baada ya awali kuonekana akiwa anahangaika kuwaokoa wanaye waliokuwa wanaishi na mke wake wa kwanza, Jennifer Garner ambaye nyumba yake ni miongoni mwa nyumba ambazo wakazi wake waliondolewa kwa lazima.
Picha zikimuonesha Ben akiwa kwenye hekaheka za uokoaji, zilisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kumfanya kuwa gumzo duniani kote.
Baadaye ‘ali-make headlines’ tena baada ya mtalaka wake, Jennifer Lopez kuonesha kuguswa na hali aliyokuwa anapitia na familia yake ya mwanzo na kueleza kuwa yupo tayari kuwasaidia kwa chochote.
Mtaa anaoishi Ben Affleck, Brentwood, licha ya kuwa jirani na maeneo yaliyoteketezwa na moto, upo salama na wananchi hawajaondolewa.