×

Morocco Yachaguliwa kuwa Makao Makuu ya Chama kipya cha vilabu vya Afrika

Rais wa Yanga na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu Afrika Eng. Hersi Said (kushoto) Aakiwa na Rais wa CAF Dr Patrice Motsepe.

Morocco imechaguliwa kuwa Makao Makuu ya Chama kipya cha Shirikisho la Vilabu Afrika Eng. Hersi Said kinachoongozwa na Rais wa Yanga Eng. Hersi Said,

BAADA ya mchakato wa ushindani wa zabuni uliohusisha Afrika Kusini, Morocco, na Algeria, Morocco iliibuka kuwa chaguo la pamoja wakati wa mkutano wa bodi ya ACA uliofanyika hivi karibuni.

Makao Makuu ya ACA yatakuwa Rabat, karibu na ofisi za shirikisho la soka la Afrika (CAF) na FIFA. Eneo hili la kimkakati litaimarisha ushirikiano na kuchangia ukuaji wa soka barani, huku Morocco ikiendelea kuchukua jukumu muhimu katika maendeleo ya soka duniani.

Kufuatia Mkutano huo, ACA ilituma barua kwa Rais wa shirikisho la soka la Morocco, Bw. Fouzi Lekjaa, kuwapongeza kwa kufanikisha zabuni hiyo.

Hii itawapa watendaji wa ACA fursa ya kuwasiliana na maafisa wa FIFA, CAF, kuhusu masuala yanayohusiana na vilabu.

ERICK MANDALA AKAMATWA na KILO 200 za COCAINE – NI BILIONEA wa CONGO ANAYEIMBWA KWENYE NYIMBO NYINGI

Leave a Comment