×

Mastaa Wapoteza Wafuasi Insta, Ronaldo Mil 8, Kylie Jenner Mil 14, Selena Gomez Mil 6 Taharuki Yaibua

Mtandao wa Instagram umeibua mjadala mkubwa duniani baada ya kuripotiwa kufanya usafi mkubwa wa akaunti fake, spam pamoja na akaunti zisizo na shughuli kupitia mfumo wa AI wa kampuni ya Meta.

Hatua hiyo ambayo watumiaji wengi wameipa jina la “Great Purge of 2026” imesababisha mastaa mbalimbali duniani kupoteza mamilioni ya followers ndani ya muda mfupi.

Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii, Kylie Jenner ameripotiwa kupoteza zaidi ya followers milioni 14, huku nyota wa soka Cristiano Ronaldo akipoteza karibu milioni 8.

Kylie Jenner

Msanii Selena Gomez naye anadaiwa kushuka kwa takribani followers milioni 6 baada ya operesheni hiyo ya kuondoa akaunti zisizo halisi.

Mastaa wengine waliotajwa kuathirika ni pamoja na Ariana Grande, Beyoncé, Taylor Swift, Justin Bieber, Virat Kohli pamoja na Priyanka Chopra.

Mashabiki wa makundi ya K-pop kama BTS na BLACKPINK pia waligundua kupungua kwa followers kwenye akaunti za makundi hayo ndani ya saa chache.

Ripoti zinaeleza kuwa Meta inalenga kupambana na akaunti bot, spam pamoja na followers wanaotokana na huduma za kuongeza followers kwa njia zisizo halali, ili kuboresha uhalisia wa engagement kwenye platform hiyo.

Mbali na mastaa wakubwa, creators wadogo na wa kati nao wameripoti kupoteza kati ya asilimia 2 hadi 5 ya followers wao katika kipindi cha saa sita pekee.

Hata hivyo, baadhi ya watumiaji wameeleza kuwa kuna uwezekano akaunti halali pia ziliathirika wakati wa operesheni hiyo kutokana na mfumo wa AI kufanya usafi mkubwa kwa wakati mmoja.

🔴 Cristiano Ronaldo
http://instagram.com/cristiano
Previous : 673,307,250
Current : 666,695,107
Change : -6,612,143 (lost)

🔴Lionel Messi
http://instagram.com/leomessi
Previous : 512,532,381
Current : 507,722,140
Change : -4,810,241 (lost)

🔴Selena Gomez
http://instagram.com/selenagomez
Previous : 414,324,851
Current : 408,836,859
Change : -5,487,992 (lost)

🔴 Taylor Swift
http://instagram.com/taylorswift
Previous : 279,993,327
Current : 275,827,600
Change : -4,165,727 (lost)

🔴 Kim Kardashian
http://instagram.com/kimkardashian
Previous : 352,635,698
Current : 347,507,844
Change : -5,127,854 (lost)

🔴 Jennifer Lopez
http://instagram.com/jlo
Previous : 245,702,759
Current : 242,271,800
Change : -3,430,959

🔴 Beyonce
http://instagram.com/beyonce
Previous : 307,211,182
Current : 302,761,202
Change : -4,449,980 (lost)

🔴 Ariana Grande
http://instagram.com/arianagrande
Previous : 371,415,576
Current : 365,838,792
Change : -5,576,784 (lost)

🔴 Priyanka Chopra
http://instagram.com/priyankachopra
Previous : 94,558,158
Current : 93,413,034
Change : -1,145,124 (lost)

🔴Katy Perry
http://instagram.com/katyperry
Previous : 200,574,213
Current : 197,583,900
Change : -2,990,313 (lost)

🔴Zendaya
http://instagram.com/zendaya
Previous : 177,281,901
Current : 175,254,149
Change : -2,027,752 (lost)

🔴 Dwayne Johnson
http://instagram.com/therock
Previous : 390,068,666
Current : 385,173,978
Change : -4,894,688 (lost)

Leave a Comment