×

Rais Samia Alivyowasili Namibia kuhudhuria hafla ya uapisho wa Rais Netumbo Nandi

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, Windhoek nchini Namibia kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya uapisho wa Rais wa nchi hiyo Netumbo Nandi-Ndaitwah tarehe 21 Machi, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, Windhoek nchini Namibia kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya uapisho wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah tarehe 21 Machi, 2025. Sherehe hizo pia zitambatana na maadhimisho ya miaka 35 ya Uhuru wa nchi hiyo ambapo Mhe. Rais Dkt. Samia amealikwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe hizo.