×

Kutoka Abuja: Makamu wa Rais Afuatilia Hotuba ya Kufunga Bunge la 12

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, ameungana na Watanzania wengine kwa njia ya mtandao kufuatilia hotuba ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuhitimisha rasmi shughuli za Bunge la 12 leo Juni 27, 2025.

Dk. Mpango yupo jijini Abuja, Nigeria, ambako anashiriki Mkutano wa 32 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (Afrexim), akimwakilisha Rais Samia katika majadiliano ya kikanda kuhusu maendeleo ya biashara na uchumi barani Afrika.