
Klabu ya Azam Fc imemtangaza Octavi Anoro kama Mtendaji Mkuu (CEO) mpya klabuni, kwa mkataba wa miaka miwili utakaombakisha hadi 2027 akichukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa Abdulkarim Nurdin maarufu kama Popat ambaye amepandishwa cheo na kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais.
Kwa mujibu wa taarifa ya leo Novemba 14, 2025 iliyotolewa na klabu hiyo Anoro (42) raia wa Hispania, anakuja na maarifa na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika nyanja ya maendeleo ya utawala na biashara ya mpira wa miguu.
Aidha, Bodi pia imemteua, Rashid Seif Mohamed, kuwa msaidizi wa Mtendaji Mkuu (Assistant CEO). Rashid ni mhitimu wa Shahada ya Umahiri ya utawala wa michezo (Master’s in Sports Management) pamoja na ngazi ya pili ya ukocha kutoka chama cha soka cha England, FA.