×

Simba Yatangaza Viingilio vya Mechi Dhidi ya Petro Atletico ya Angola

Dar es Salaam, Tanzania — Klabu ya Simba SC imetangaza viingilio vya mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya Petro Atletico ya Angola, utakaochezwa Jumapili, Novemba 23, 2025, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akitangaza taarifa hiyo, Meneja wa Habari wa klabu hiyo, Ahmed Ally, amesema viingilio vimepangwa kwa kuzingatia mahitaji ya mashabiki na ukubwa wa mchezo huo wa kimataifa.

Kwa mujibu wa Ahmed, tiketi za mzunguko zitauzwa kwa Tsh 5,000, huku maeneo ya VIP yakiwa na viwango vifuatavyo:

  • VIP C: Tsh 10,000

  • VIP B: Tsh 20,000

  • VIP A: Tsh 30,000

Kwa mashabiki wanaotaka huduma za juu zaidi, tiketi za Platinum zitapatikana kwa Tsh 150,000, wakati tiketi za hadhi ya juu zaidi—Tanzanite—zitauzwa kwa Tsh 250,000.

Simba SC imewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao katika mchezo huo muhimu wa kuwania nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Leave a Comment