×

Mbunge Baba Levo Ataka Madiwani na Mkurugenzi Kuacha Kuingiliana Kazi

MBUNGE wa Kigoma Mjini, Clayton Chipando ‘Baba Levo’, ametoa onyo kali dhidi ya migogoro inayoibuka kati ya madiwani na wakurugenzi, akisema ni “sumu kubwa” inayokwamisha juhudi za maendeleo katika Halmashauri na Manispaa.

Ametoa kauli hiyo Desemba 2, 2025, wakati akizungumza katika Baraza la Kwanza la Madiwani wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, ambako alipata fursa ya kusalimia na kutoa nasaha zake kwa viongozi hao.

Baba Levo amesema amekuwa akifuatilia kwa ukaribu mienendo ya baadhi ya vikao na mahusiano ya kazi kati ya madiwani na Mkurugenzi wa Manispaa, Kisena Mabuba, na kusisitiza kuwa ushirikiano kati ya pande hizo mbili ni muhimu kuliko tofauti zao.

“Ugomvi wa madiwani na wakurugenzi ni sumu kwa maendeleo. Tusipoelewana, wananchi ndio wanaoumia. Tukishirikiana, maendeleo yanapatikana kwa kasi,” amesema Baba Levo.

Ameongeza kuwa endapo kutajitokeza malumbano au mvutano usio na tija, hatasita kulifikisha suala hilo kwa Rais Samia Suluhu Hassan ili hatua zichukuliwe kwa masilahi ya wananchi.

Mbunge huyo pia ameonyesha imani kubwa kwa Mkurugenzi Mabuba, akiwataka madiwani kumpa ushirikiano wa kutosha ili kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

MWANA-FA MSIBANI kwa MAMA wa CRAZY GK – AFICHUA WALIVYOTUPIWA CHUPA STEJINI….

Leave a Comment