Video Vixen Genno Acharuka “Nilikopwa Kwenye Video ya Diamond na Baba Levo” – Video

Video vixen maarufu Genno ameibua gumzo baada ya kufichua kuwa aliwahi kukopwa malipo katika moja ya video aliyocheza akiwashirikisha wasanii wakubwa, akiwemo Diamond Platnumz na Baba Levo.
Genno amesema alipata nafasi hiyo kupitia mwandaaji wa video ambaye hakutaka kumtaja jina, lakini licha ya kufanya kazi kwa weledi, hakuwahi kulipwa kama walivyokubaliana.
Vixen huyo ambaye amekuwa akitokea kwenye video nyingi za wasanii wakubwa kama Harmonize, Balaa MC na wengine, amefunguka mambo mengi kuhusu safari yake ya kazi, changamoto anazokutana nazo, pamoja na namna tasnia ya video vixens ilivyo na changamoto nyingi zisizoonekana hadharani.
Katika mahojiano hayo, Genno pia ametumia nafasi hiyo kuwashauri vijana kuzingatia kazi zao na kutumia muda wao kujijenga badala ya kujiingiza kwenye mambo yasiyo na tija.
“Vijana muda ni mali, tumieni vipaji vyenu kujenga maisha yenu. Tusipoteze nguvu kwenye vitu ambavyo havitusaidii,” amesema.
Kauli yake imepokelewa kwa hisia tofauti, huku mashabiki wengi wakimsifia kwa ujasiri na uwazi.

