The House of Social Media
gunners X

Wizara ya Maliasili na Utalii Yatangaza Nafasi za Kazi Dodoma

0

Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT) inatangaza nafasi za ajira kupitia Mradi wa Food Systems, Land Use and Restoration in Tanzania’s Forest Landscapes, sehemu ya mpango mpana wa kimataifa wa GEF FOLUR Impact Program. Mradi huu wa miaka mitano unatekelezwa kwa ushirikiano na World Wildlife Fund (WWF) kama GEF Implementing Agency.


Kuhusu Mradi

Mradi unalenga kukabiliana na mmomonyoko wa mazingira, hususan misitu na maeneo oevu, unaosababishwa na shughuli za kilimo—hasa uzalishaji wa mpunga. Tanzania ni mzalishaji wa pili wa mpunga Kusini Mashariki mwa Afrika, lakini bado uzalishaji ni mdogo kutokana na changamoto za miundombinu, uzalishaji mdogo kwa hekta (tani 1.5–2), na misururu ya uzalishaji isiyo na ufanisi.

Mradi unatekelezwa katika mandhari mawili muhimu kwa kilimo cha mpunga:

  • Bonde la Kilombero (Tanzania Bara)

  • Kaskazini Unguja (Zanzibar)

Mradi unajikita katika nguzo tatu kuu:

  1. Integrated Landscape Management kupitia ushirikishwaji wa wadau.

  2. Uendelezaji wa mifumo endelevu ya mnyororo wa thamani wa mpunga.

  3. Urejeshwaji wa mandhari na maeneo muhimu ya kimazingira.


NAFASI YA KAZI 1: Sustainable Food Systems Specialist – Rice Sector Development

Eneo: Dodoma
Muda: Mwaka 1, unaoweza kuongezeka hadi miaka 4
Anaripoti kwa: Project Coordinator, FOLUR Project (MNRT)

Majukumu Makuu

  • Kuongoza utekelezaji wa Component 2 ya mradi—mnyororo wa thamani wa mpunga.

  • Kuandaa sera na miongozo kuhusu:

    • Umiliki wa ardhi na utawala wa maji,

    • Mnyororo wa thamani wa mpunga,

    • Viwango, kanuni na mafunzo kwa wadau wa sekta.

  • Kufanya uchambuzi wa fursa za uwekezaji wa sekta binafsi.

  • Kusimamia ushirikiano baina ya serikali, sekta binafsi na wadau wa kiraia.

  • Kupitia ripoti za wataalamu/washirika na kuhakikisha ubora wa kazi.

  • Kufanya ziara za ufuatiliaji na kutoa mwongozo wa kiufundi.

  • Kuchangia maandalizi ya ripoti za mradi.

  • Kusimamia ushiriki wa makundi ya wakulima na wadau wengine.

  • Kuhakikisha utekelezaji unafuata taratibu za GEF na WWF.

  • Kuliwakilisha mradi kwenye mikutano na warsha.

Sifa za Mwombaji

  • Uzoefu wa miaka 5+ katika sekta ya mifumo ya chakula, hususan mpunga.

  • Shahada ya Uzamili katika: Agricultural Engineering, Agronomy, Crop Science, Agribusiness au fani inayohusiana.

  • Uwezo wa kufanya kazi na wadau wa ngazi ya juu (serikali, sekta binafsi na NGOs).

  • Uzoefu wa kusimamia miradi yenye wadau wengi.

  • Uzoefu na miradi ya GEF ni faida.


NAFASI YA KAZI 2: Gender and Safeguards Specialist

Eneo: Dodoma
Muda: Mwaka 1
Anaripoti kwa: Project Coordinator, FOLUR Project

Majukumu Makuu

Environmental & Social Safeguards

  • Kuhakikisha nyaraka za zabuni/mikataba zinajumuisha matakwa ya kimazingira na kijamii (ESMF, GAP, SEP).

  • Kusimamia tathmini na udhibiti wa hatari za kijamii na kimazingira.

  • Kuandaa ESMPs kwa maeneo maalum ya mradi.

  • Kufuatilia utekelezaji wa kanuni za ulinzi na kutoa mafunzo kwa PMU na LCUs.

  • Kutengeneza zana za urahisishaji kama fomu na checklist.

  • Kushiriki ziara za pamoja za ufuatiliaji.

  • Kusimamia uanzishaji wa Grievance Redress Mechanisms (GRM).

  • Kutoa mchango kwenye ripoti za robo mwaka, nusu mwaka na mwaka.

Gender Mainstreaming & Stakeholder Engagement

  • Kuongoza utekelezaji wa Gender Action Plan (GAP).

  • Kusimamia utekelezaji wa Stakeholder Engagement Plan (SEP).

  • Kutoa mafunzo kuhusu ujumuishaji wa kijinsia kwa timu za mradi.

  • Kuhakikisha bajeti na mipango ya kazi yanazingatia ushiriki wa wanawake, vijana na makundi maalum.

  • Kushauri kuhusu hatari kama ukatili wa kijinsia (GBV/SEA/SH).

  • Kuhakikisha usawa wa jinsia unazingatiwa katika warsha, mafunzo na shughuli za ufieldi.

  • Kusaidia kuandaa taarifa, ripoti na nyaraka za matokeo.

Sifa za Mwombaji

  • Uzoefu wa miaka 5+ katika Gender Mainstreaming na/au Safeguards.

  • Shahada ya Uzamili katika Social Sciences, Gender Studies, Community Development au fani zinazohusiana.

  • Uzoefu katika kutoa taarifa kwa miradi kubwa, hususan inayofadhiliwa na wafadhili.

  • Uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza na Kiswahili.

  • Uzoefu na miradi ya GEF ni faida.


Masharti ya Jumla Kwa Waombaji

  1. Awe Mtanzania, chini ya miaka 50.

  2. Aambatanishe CV ya kisasa yenye anwani, simu na email.

  3. Aombe kwa kutegemea taarifa katika tangazo hili.

  4. Aambatanishe nakala zilizothibitishwa za:

    • Vyeti vya elimu (degree, diploma n.k.),

    • Transcripts,

    • Cheti cha kuzaliwa,

    • Vyeti vya usajili wa kitaalamu (ikiwa vinahusika).

  5. Haitakubaliwa: Result slips, testimonials na partial transcripts.

  6. Watumishi wa umma waombe kupitia kwa waajiri wao.

  7. Wastaafu hawaruhusiwi kuomba.

  8. Wasilisha majina ya referee watatu.

  9. Vyeti vya nje vihakikiwe na NECTA, TCU au NACTE.

  10. Barua ya maombi isainishwe na iandikwe Kiingereza au Kiswahili.

  11. Anwani ya kutuma maombi:

Permanent Secretary
Ministry of Natural Resources and Tourism
Government City – Mtumba, Ardhi Street
P.O. Box 1351,
DODOMA

  1. Mwisho wa kutuma maombi: 10 Desemba 2025

  2. Waliochaguliwa tu watapewa taarifa ya usaili.

  3. Wasilishaji wa nyaraka za kughushi utachukuliwa hatua za kisheria.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MKATABA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII 04-12-2025

Leave A Reply