The House of Social Media
gunners X

Katambi Ateuliwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Makonda Wizara ya Habari

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri kwa kuwateua na kuwabadilisha baadhi ya viongozi wa serikali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, Patrobas Paschal Katambi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, akichukua nafasi ya Boniface George Simbachawene ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Katika mabadiliko hayo, Rais Samia pia amemteua Paul Makonda kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huo, Makonda alikuwa Naibu Waziri wa wizara hiyo. Waziri aliyekuwa akiongoza wizara hiyo, Profesa Palamagamba John Aidan Kabudi, ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Ikulu (Kazi Maalum).

Aidha, taarifa hiyo ya Ikulu iliyotolewa Januari 8, 2026, imeeleza kuwa Rais Samia amemteua Waziri Rajab Salum kuwa Balozi.

Mabadiliko hayo ni sehemu ya jitihada za Rais Samia kuimarisha utendaji kazi wa serikali na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Leave A Reply