×

Mkazi wa Bunju Aibuka Mshindi wa Mil. 50, za Magift ya Mixx Pesa

Bw. Yusuph Constantine Muhoja akiwa kwenye pozi la furaha kwenye hafla ya kumtangaza.

14 Januari 2026 – Dar es Salaam;– Mkazi wa Bunju jijini Dar es Salaam, Bw. Yusuph Constantine Muhoja ameibuka mshindi wa jumla wa milioni 50 kwenye Kampeni ya mwisho wa mwaka ya Magift ya Mixx Pesa kutoka Mixx.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Bi. Angelica Pesha, (kushoto) akimpongeza mshindi, kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas, Bw. Pierre Canton Bacara na mwenye hijab nyeusi ni mke wa mshindi.

Hafla ya kufunga kampeni hiyo, imehudhuriwa na viongozi waandamizi wa Yas na Mixx akiwemo Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas, Bw. Pierre Canton Bacara na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Bi. Angelica Pesha, wateja na wadau wa kibiashara wa Yas na Mixx.

Mshinjdi na mkewe wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Yas na Mixx

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hiyo kwa mshindi wa jumla wa Kampeni hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Bi. Angelica Pesha, alisema kuwa

Kampeni ya ‘Magifti ya Mixx Pesa’ imegusa maisha ya watanzania kwa namna ya kipekee. Tumewaona kina mama wakilipa ada za watoto, vijana wakikuza biashara zao, na familia zaidi ya 40 zikianza mwaka mpya kwa matumaini mapya. Hii ndiyo maana ya kuwa mshirika halisi wa kifedha kwa watanzania,” alisema.

Kupitia kampeni hii, Mixx imeweza kuibua zaidi ya Ma-Mixxionea 44 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania, wakiwemo:

  • Washindi 37 wa TSh 1 milioni
  • Washindi 5 wa TSh 5 milioni
  • Mshindi 1 wa TSh 10 milioni
  • Na mshindi mkuu wa TSh 50 milioni, Ndugu Yusuph Constantine Muhoja

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Biashara Mixx, Bw. James Sumari, alisisitiza dhamira ya Mixx ya kutimiza ahadi zake:

Leo tunafunga kampeni yetu ya Magift ya Mixx Pesa, lakini hatufungi safari ya Mixx. Kampeni hii imekua sehemu kubwa ya ahadi yetu ya kuwa mshirika wa karibu wa kifedha kwa kila Mtanzania – kupitia huduma za malipo, mikopo, akiba, na huduma nyingine za kidijitali. Tumeshuhudia zawadi zikibadilisha maisha ya watanzania. Tunajua fedha tulizokabidhi, zitafungua milango mipya ya mafanikio, na tunajivunia kuwa sehemu ya safari hiyo.”

Leave a Comment