The House of Social Media
gunners X

Zambia Yadhibiti Matumizi ya Dola, Kwacha Yapaa Afrika

0

Kwa sasa, Kwacha ya Zambia inatajwa kuwa miongoni mwa sarafu zinazofanya vizuri zaidi barani Afrika dhidi ya Dola ya Marekani, hali iliyozua mjadala mpana kuhusu sababu za mafanikio hayo.

Moja ya sababu kuu ni sekta ya madini ya shaba (copper). Zambia ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa shaba barani Afrika, nyuma ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na imo kwenye nchi 10 bora duniani kwa uzalishaji wa madini hayo. Biashara ya shaba huingiza kiasi kikubwa cha fedha za kigeni, hali inayoongeza nguvu ya sarafu ya taifa.

Sababu ya pili, na inayotajwa kuwa ya msingi zaidi, ni sera kali ya fedha iliyopitishwa na Zambia ya kupunguza na hatimaye kuondoa matumizi ya dola ya Marekani katika miamala ya ndani. Marufuku ya kutoza na kulipa kwa dola ndani ya nchi imeongeza mahitaji ya Kwacha, hivyo kuchangia kuimarika kwa thamani yake.

Hatua kama hiyo pia imeanza kuchukuliwa na Tanzania, ambapo Serikali imeanza kupiga marufuku matumizi ya dola katika malipo na tozo za ndani, isipokuwa kwa sababu maalum na kwa taasisi zilizoainishwa kisheria.

KHAMENEI AMLAUMU VIKALI TRUMP KWA KUCHOCHEA MAANDAMANO YALIYOSABABISHA MAUAJI 📍IRAN

Leave A Reply