The House of Social Media
gunners X

Serikali Yatenga Bilioni 25, Maeneo Maalum Ya Uwekezaji Viwanda Vya Dawa

0
Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa

Serikali imetenga maeneo maalum la uwekezaji wa viwanda vya bidhaa za afya pamoja na kutenga kiasi cha zaidi ya Bilioni 25 (Dola Milioni zaidi ya milioni 10 za kimarekani) ikiwa ni mkakati mojawapo wa kuimarisha uwekezaji na uzalishaji wa ndani wa dawa, chanjo na vifaa tiba ili kuifungua Tanzania kuwa miongoni mwa wazalishaji vinara wa bidhaa hizo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa akizungumza na wawekezaji wa bidhaa za afya kutoka ndani na nje ya nchi wenye nia ya kufanya uwekezaji wa Viwanda vya kuzalisha bidhaa za afya, leo Januari 19, 2026 Jijini Dar es Salaam.

“Serikali imedhamiria kuimarisha uzalishaji wa bidhaa za afya nchini, kwa kuzingatia hilo, leo natangaza rasmi kuwa Serikali imetenga eneo sehemu ya Mloganzila na Kibaha kwa ajili ya wawekezaji wa bidhaa hizo” amesema Waziri Mchengerwa.
Amebainisha kuwa maeneo hayo yatawezeshwa kwa miundombinu bora, itakayowaunganisha pamoja wawekezaji, usimamizi thabiti pamoja tafiti na maendeleo ya bidhaa za afya yatakayochangia kupunguza gharama za uzalishaji na kuharakisha uzalishaji unaokidhi viwango vya kimataifa.

Katika kuunga mkono juhudi za uwekezaji wa viwanda vya bidhaa za afya, Serikali pia imetangaza kutoa Dola za Marekani milioni 10 kwa ajili ya kuanzisha Maabara ya pamoja ya dawa (Shared Pharmaceutical Laboratory Facility) itakayohudumia maeneo yote.

“Maabara hiyo itatoa huduma za upimaji wa ubora, tafiti za bio-equivalence, na msaada wa udhibiti, hatua itakayopunguza vikwazo kwa wawekezaji, kuharakisha kuingia sokoni kwa bidhaa, na kuimarisha uzingatiaji wa viwango vya WHO Prequalification na GMP” amefafanua Waziri Mchengerwa.

KOCHA SENEGAL ALIYEHAMASISHA WACHEZAJI KUGOMA -CAF WAMCHUKULIA HATUA – ANAWEZA KUKOSA KOMBE LA DUNIA

Leave A Reply