
Klabu ya Sekhukhune United ya Afrika Kusini imetuma rasmi maombi ya kumtaka winga wa Yanga SC, Cesestine Ecue, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.
Kwa taarifa zilizopatikana, mazungumzo yanaendelea kwa sasa baina ya Yanga SC na Sekhukhune United kuhusu dili hilo la kumkopa Ecue, huku pande zote mbili zikiwa katika hatua za kujadili masharti ya mkopo huo.
Hadi sasa hakuna taarifa rasmi kutoka kwa Yanga SC au Sekhukhune United kuhusu maendeleo ya mazungumzo hayo, lakini vyanzo vya ndani ya klabu vinadai kuwa pande zote zinatafakari kwa makini ili kuhakikisha maamuzi yanayofanywa ni mazuri kwa pande zote na haswa kwa wachezaji.
Ecue amekuwa mmoja wa wachezaji wanaotarajiwa kuwa na mchango mkubwa kwa Yanga msimu huu, hivyo uamuzi wa kumkopa au kumuweka katika kikosi utategemea muktadha wa timu na mpango wa kocha katika kipindi cha msimu.

