
Wakazi na wanariadha wilaya ya Moshi na mkoani Kilimanjaro kwa ujumla wana kila sababu ya kutabasamu kufuatia uzinduzi wa msimu wa 24 wa mbio maarufu za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon 2026 uliofanyika hoteli ya Salinero iliyoko Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Kiseo Yusuf Nzowa aliyewakilishwa na Afisa Michezo wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Anthony Ishumi, alisema tukio hilo kwa miaka mingi limechangia kwa kiasi kikubwa kuutangaza Mkoa wa Kilimanjaro na kuiweka Tanzania kwenye ramani ya duniani linapokuja swala la mbio za kimataifa.

“Sote tunajua jinsi mbio za Kilimanjaro Marathon zilizvyochangia ukuaji wa uchumi wa wilaya ya Moshi na Mkoa wa Kilimanjaro kw aujumla kupitia utalii wa michezo”, alisema.
Aliendelea kubainisha kuwa ukweli kwamba mbio za Kilimanjaro Marathon huvutia zaidi ya washiriki 13,000 na idadi ya watazamaji kutoka zaidi ya nchi 60 duniani kote ambapo alisema katika kuadhimisha msimu wake wa 24 mbio hizo zinakuwa ni kongwe zaidi ya mbio zingine za nyika hapa nchini.
“Mbio hizi zimeandaliwa kwa msimu wa 24 sasa na zimeleta mafanikio ya kiuchumi kwa familia nyingi mjini Moshi na miji mingie ya Jirani kutokana na kukua kwa biashara, ambapo Pamoja na mambo mengine hotel izote huwa zinajaa kutokanana wageni wengi wanaofika wakati wa tukio hili muhimu kwenye kalenda michezo hapa nchini”, alisema.
Alitoa wito kwa wafanyabiashara wilayani Moshi na mkoani Kilimanjaro kw aujumla kutumia fursa ya mbio hizo kukuza biashara zao ambapo alitoa rai kwa wafanyabiashara hao kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wageni watakoakuwa Moshi kipindi chote cha mbio hizo.
“Ninawapongeza wadhamini wote wanaoongozwa na Kilimanjaro Premium Lager (mdhamini mkuu wa mbio za kilomita 42), YAS ambao ni wadhamini wa Kilomita 21 (Kili Half Marathon), Benki ya CRDB ambao ni wadhamini wa mbio za kujifurahisha za kilomita 5, kwa kufanikisha tukio hili”, alisema.
Aliwapongeza wadhamini wengine ambao alisema ni Pamoja na Kilimanjaro Water, TPC Sugar,GardaWorld Security, Toyota Tanzania, Columbia Sportswear, Simba Cement, Harleys Healthcare Solutions, ALAF Limited, Hoteli ya Salinero,Kibo Palace Hotels ya Jijini Arusha na Keys Hotels a mjini Moshi.
“Pia tungependa kuwashukurumakampuni yatakayofanya maonyesho ya bidhaa mbalimbali wanazozalilsha ikiwa ni sehemu ya tukio hili muhimu; nimetaarifiwa huwa watafanya maonyesho hayo kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha uhsirika Moshi (MoCU) kati ya Machi 21 hadi Machi 23”, alisema na kuongeza, nitoe rai kwa washiriki na wale wote watakaokuweko Moshi kipindi chote cha mbio hizi kuwauna mkono wafanyabiashara kwa kutembelea maonyehso hayo.
“Kampuni ambazo tayari zishajiorodhsha kwa ajili ya kufanya maonyesho hayo kuwa ni Pamoja na HiSense, Ruwenzori Marathon, Schultz Sportreisen, Bodi ya Kahawa ya Tanzania (TCB), Huduma ya Afya ya DKT, kampuni ya Uhasibu ya Enson Africa Chartered, Nyikani Trails, Bodi ya Utalii ya Tanzania (TTB) na Graph X”, alisema na kuongeza uchiriki wenu utachangia kuboresha tukio hili la kimataifa.
Mkurugenzi wa Masoko wa Tanzania Breweries Limited (TBL), Khensani Mkhombo, alisema kampuni hiyo inajivunia kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa mbio hizo kwa msimu wa 24 mfululizo jambo ambalo alisema limeifanya kampuni hiyo kuwa mdhamini wa muda mrefu kwenye sekta ya michezo kuliko mdhamini mwingine yeyote Hapa nchini Tanzania.
“Kupitia udhamini wa mbio hizi kampuni yetu imetoa mchango mkubwa sana katika kukuza utalii wa nchi Pamoja na uchumi wa Taifa kwa ujumla kutokana na mbio hizi kushirikisha watu kutoka maeneo malimbali duniani kote”, alisema.
Alitoa rai kwa wale wote wanaotarajia kushiriki bio hizo kujianikisha mapema kupitia ukurasa rasmi ya kujisajili ulioko kwenye tovuti ya www.kilimanjaromarathon.com na pia kupitia Mixx BY YAS.
Alisema ndani ya wiki ya tukio hilo kutakuwa na shughuli za kufurahishaambapo alitoa rai kwa washiriki sambamba na wageni wengine kupanga kukaa muda mrefu katika mji wa Moshi ili waweze kufurahia ukarimu wa wadhamini wakuu Kilimanjaro Premium Lager pamoja na shughuli zingine zitakazoendana na tukio hilo.
“Kuanzia Ijumaa hadi siku ya mbio hizo ambayo ni Jumapili, tunatarajia kuandaa Matamasha ya Kilimanjaro Lager, tuna uhakika wateja wetu watafurahishwa na kuvutiwa na matukio ya kufurahisha yanayotarajia kuchukua ziku 3 wakati wa tukio la mbio hizo”, alisema na kuongeza, matukio hayo yatakuwa pia yanalenga kuunga mkono wafanyabiashara walioko Moshi.
Akizungumzia kuhusu mbio hizo, Mkhombo alisema zawadi kwa mbio za kilomita 42 zitakuwa ni 5,500,000/- kwa washindi wa kwanza kwa washiriki wanaume na wanawake.
“Mshindi wa pili wa kiume na wa kike wanatarajiwa kuzawadiwa 2,800,000/-, ambapo kwa mshindi wa tatu Zawadi ni 1,450,000/-, mshindi wa nne, 1,150,000/-, mshindi wa tano – 900,000/-, mshindi wa sita725,000, mshindi wa saba -650,000/-, mshindi wa nane 600,000/- Mshindi wa tisa 475,000/- na mshindi wa kumi 425,000”, alisema.
Aidha alisema pia kutakuwa na Zawadi ya mshindi mkongwe wa umri kati ya miaka 40-49 ambaye atapata Zawadi ya 220,000/- na mkongwe wa umri kati ya miaka 50-59 atapokea Zawadi ya 220,000/- na Mtanzania wa kwanza atapata bakshishi ya 600,000/-.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa YAS na MIXX, Bw. Shaibu Hamisi alisema, “YAS inajivunia kwa kuendelea kuwa mdhamini rasmi wa Kilimanjaro International HalfMarathon kwa msimu wa 11; ushirikiano huu unadhihirisha mchango mkubwa unaotolewa na kampuni yetu katika kuwezesha jamii hapa nchini Tanzania”.
“Tukiwa ni moja ya mshirika muhimu katika maendeleo ya taifa, tunaendelea kutoa michango yetu mbalimbali katika kukuza vipaji, sekta ya utalii, pia kuunga mkono mipango inayplenga kukuza sekta ya afya na pamoja na Uchumi wa Taifa kupitia teknolojia yetu bora zetu bora za 4G na 5G”, alisema.
Aliongeza, “Nitoe rai kwa watu wote kuungana nasi kwa kushiriki mbio hizi sambamba na kusherehekea tukio hili muhimu nchini Tanzania kupitia mtandao wa YAS katika mbio za Kilimanjaro Marathon ya 2026”
Kuhusu zawadi za YAS 21km (Kili Half Marathon) kwa Wanaume na Wanawake alisema kuwa mshindi wa kwanza wa kiume na wa kike watazawadiwa 3,400,000/- kila mmoja ambapo mshindi wa pili atapata Zawadi ya 1,700,000/- kila mmoja.
Kuhusu Mshindi wa tatu, alisema Zawadi zitakuwa ni 1,200,000/- kwa washindi wa kiume na wa kike, Mshindi wa nne 1,000,000/-, Mshindi wa tano 850,000/-, Mshindi wa sita 700,000, Mshindi wa saba 550,000/-, Mshindi wa nane 500,000/-, Mshindi wa tisa 450,000/- na Mshindi wa kumi 400,000.
Aidha alisema kuwa Yas pia itatoa Zawadi kwa washindi wakongwe ambapo mshindi katika kitengo cha umri kati ya miaka 40-49 atapokea Zawadi ya 200,000/-, Mshindi wa kile cha umri kati ya 50-59 anatarajiwa kupokea Zawadi ya 200,000/- na Mtanzania wa kwanza akipokea bakshishsi ya 500,000/-.
Meneja wa Biashara Kanda ya Kaskazini wa Benki ya CRDB, Bw. Emmanuel Kafui, ambaye benki yake inadhamini mbio za Km 5, alisema, “Iwapo utajiuliza kwa nini Benki ya CRDB inadhamini mbio hizi za Kili Marathon basi jibu ni rahisi tu. Ukweli ulio wazi ni kwamba sote hapa tunafahamu kuwa Kili Marathon ni mbio zinazowaleta watu wengi pamoja na ni nyenzo ya kuutangaza utalii wa Tanzania kwani washiriki hutoka ndani ya nchi, Afrika Mashariki, Afrika na duniani kote kwa ujumla.”
Alisema kwa kuwa mbio hizo huwakutanisha maelfu ya wakimbiaji, Benki ya CRDB ambayo wakati wote inawajali wateja wake, imeona ni fursa muhimu kuzifadhili ili kudumisha furaha ya wateja wao wanaoshiriki pamoja na Watanzania na wageni wote wanaoenda kujumuika nao. Kwa upande wao, waandaaji wa tukio hilo wametoa rai kwa washiriki wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Machi 22, mwaka huu, kufanya usajili wao mapema ili kuepuka changamoto ya kutafuta usajili dakika za mwisho.
“Wanaotarajia kushiri watambue ya kuwa nafasi za ushiriki, ambapo washiriki watapata huduma ya anaefika wa kwanza atahudumiwa kwanza; idadi iliyopangwa ikiamilika mfumo wa usajili utafungwa”, alionya.
Mashindano ya Kimataifa ya mbio za Kilimanjaro Premium Lager, ambayo yatafanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika cha Moshi (MoCU), yameandaliwa na Kampuni ya Kilimanjaro Marathon Limited ambapo kampuni ya Wild Frontiers inawajibika na shughuli zote zinazohusiana na mbio hizo ikiwemo maswala ya usafiri wa ndani Pamoja maswala yote yanayohusiana na masoko Pamoja na matangazo ndani na nje ya nchi.