The House of Social Media
gunners X

Ligi Kuu Bara Yashika Nafasi ya 6 Afrika, Yapanda hadi Nafasi ya 54 Duniani

0

Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara imeendelea kuimarika kimataifa baada ya kushika nafasi ya sita (6) kwa ubora barani Afrika na nafasi ya 54 duniani, kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizotangazwa juma hili.

Licha ya kushuka kwa nafasi mbili Afrika ikilinganishwa na mwaka 2024, Ligi Kuu ya Tanzania imeonyesha maendeleo makubwa kimataifa kwa kupanda nafasi tatu duniani, kutoka nafasi ya 57 mwaka 2024 hadi nafasi ya 54 mwaka 2025.

Aidha, alama za ubora wa Ligi hiyo zimeongezeka kwa kiwango kikubwa, kutoka alama 266.75 mwaka 2024 hadi kufikia alama 308.5 mwaka 2025, hatua inayodhihirisha kuongezeka kwa ushindani, mvuto na ubora wa mashindano.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imewashukuru wadau wote wa Ligi hiyo, wakiwemo vilabu, wachezaji, makocha, waamuzi, wadhamini pamoja na mashabiki, kwa mchango wao mkubwa uliosaidia Ligi Kuu ya NBC kuendelea kuwa miongoni mwa Ligi bora na zenye mvuto barani Afrika.

Hatua hiyo inaonesha mwelekeo chanya wa soka la Tanzania, huku matarajio yakiwa ni kuendelea kupanda zaidi katika viwango vya ubora barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Leave A Reply