Rais Samia Apanda mti Bungi Kilimo, Zanzibar kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa – Video


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amepanda mti katika eneo la Bungi Kilimo, Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.
Mti huo ambao ni wa aina ya Mangifera indica kitaalamu, unaofahamika kwa jina la Mwembe Shomari, umepandwa leo Januari 27, 2026
tarehe ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais Samia.
Tukio hilo limefanyika sambamba na Kampeni ya 27 ya Kijani, inayolenga kuhamasisha upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira ili kuifanya Tanzania kuwa ya kijani.


