×

Waumini Wajitokeza Kuaga Mwili Kardinali Pengo Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu – (Picha+Video)

 

Waumini na viongozi mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kuuaga mwili wa Polycarp Pengo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu jijini Dar es Salaam.

Ibada ya kuaga imeambatana na huzuni, vilio na sala maalum za kumuombea marehemu, huku waumini wakikumbuka mchango wake mkubwa katika kuliongoza Kanisa Katoliki na kulihudumia taifa kwa ujumla.

Viongozi wa dini na serikali walihudhuria kutoa heshima zao za mwisho, wakieleza kuwa Kardinali Pengo ameacha alama isiyofutika katika historia ya Kanisa na jamii.

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alifariki dunia Februari 19, 2026 alipokuwa akipata matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI na atazikwa Jumamosi Februari 28, 2026 katika kituo cha Hija Pugu, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Leave a Comment