
Benki ya Absa Tanzania imeendelea kuimarisha ushirikiano wake na wateja kwa kuandaa hafla ya futari iliyowakutanisha viongozi wa benki, viongozi wa dini, wafanyakazi pamoja na wateja, hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, alisema benki hiyo inaendelea kuthamini uhusiano wake na wateja na wadau mbalimbali, huku akisisitiza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kukuza huduma bora za kifedha na maendeleo ya jamii.
Miongoni mwa wageni waliohudhuria katika hafla hiyo ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Alhad Omar, ambaye alikuwa mgeni rasmi, baadhi ya wakurugenzi wa benki hiyo pamoja na wafanyakazi..
Hafla hiyo ya futari imeelezwa kuwa ni sehemu ya utamaduni wa Benki ya Absa Tanzania wa kuendelea kujenga ukaribu na wateja wake pamoja na kuimarisha mshikamano na jamii.
