×

Waziri Mkuu Mwigulu Aeleza Masikitiko Yake Kufuatia Kifo cha Lukuvi – Video

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba.

Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba, ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha William Vangimembe Lukuvi kilichotokea leo Machi 25, 2026.

Waziri Mkuu Nchemba alitoa salamu hizo akiwa katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (PICC), alikokuwa akishiriki Mkutano wa 110 wa Wadau wa Elimu kwa Umma (WASHITIRI), ambapo alieleza masikitiko yake kutokana na msiba huo mkubwa wa kitaifa.

Taarifa rasmi ya kifo cha Lukuvi ilitangazwa na Rais Samia, ambaye alieleza kuwa marehemu amefariki dunia majira ya saa moja asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

Katika salamu zake, Rais Samia ametuma pole kwa Spika wa Bunge, familia ya marehemu, wananchi wa Jimbo la Isimani pamoja na Watanzania wote kwa ujumla kutokana na msiba huo.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Nchemba ameungana na viongozi wengine wa serikali na wananchi katika kuomboleza kifo hicho, akisisitiza kuwa taifa limepoteza kiongozi mwenye mchango mkubwa katika utumishi wa umma na uongozi wa nchi.

Kifo cha Lukuvi kimeendelea kuibua huzuni miongoni mwa Watanzania, huku viongozi mbalimbali wakitoa salamu za pole na kuungana na familia, marafiki na wananchi wa Isimani katika kipindi hiki cha maombolezo.

Viongozi wa serikali wameendelea kutoa wito wa mshikamano na subira wakati taifa likiomboleza kiongozi huyo mkongwe aliyelitumikia kwa muda mrefu katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Leave a Comment