×

Askofu Mkuu Mpya Aonyesha Heshima kwa Familia ya Kifalme

Sarah Mullally, Askofu Mkuu mpya wa Church of England, alionyesha ishara ya heshima kwa Prince William na Kate Middleton wakati wa hafla yake ya kuapishwa iliyofanyika katika Canterbury Cathedral.

Tukio hilo lilifanyika Machi 25, ambapo Prince William na Princess Kate walihudhuria kwa niaba ya Mfalme King Charles III. Katika video zilizosambaa mitandaoni, Mullally alionekana kusitisha msafara wake na kuinama kidogo (bow) kama ishara ya heshima kwa wanandoa hao wa kifalme, ambao walikuwa wakishiriki hafla hiyo pamoja na wageni wengine.

Prince William na Kate Middleton walijibu kwa tabasamu, huku Princess Kate akitikisa kichwa kwa heshima kabla ya Mullally kuendelea na msafara wake.

Tukio hilo limeibua umakini mkubwa kutokana na umuhimu wa uhusiano wa karibu kati ya Kanisa la England na familia ya kifalme, ambapo Askofu Mkuu wa Canterbury ana majukumu muhimu ikiwa ni pamoja na kuongoza sherehe za kitaifa kama vile kutawazwa kwa mfalme, ndoa za kifalme, pamoja na matukio mengine ya kihistoria.

Uteuzi wa Sarah Mullally unamfanya kuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya zaidi ya miaka 1,400 kuongoza kanisa hilo, hatua inayochukuliwa kama mabadiliko makubwa ndani ya taasisi hiyo ya kidini na kihistoria.

Katika hafla hiyo pia, wawili hao wa kifalme walipata muda wa kuzungumza na Mullally, hali inayoonesha uhusiano unaoendelea kati ya viongozi wa kanisa na familia ya kifalme nchini Uingereza.

Leave a Comment