×

Video: Polisi Ruvuma Wawakamata Watuhumiwa wa Mauaji ya Dereva Bodaboda

Kamanda wa Mkoa wa Ruvuma Chilya (SACP) akizungumza na waandishi wa habari

Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linawashikilia watuhumiwa wawili, Saidi Ramadhani (28), mkazi wa Mshangano–Namanyigu, na Gamaliel Mundo (36), mkazi wa Mtyangimbole, kwa tuhuma za kumuua Lucas Msongela (32), dereva bodaboda na mkazi wa Mkuzo, Songea.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Machi 18, 2026 majira ya usiku, baada ya kumteka mwendesha pikipiki huyo na kumpeleka eneo la Peramiho, kisha kumshambulia kwa kutumia kitu butu na kusababisha kifo chake.

Baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma lilianza msako maalum kwa kutumia timu ya wataalamu wa uchunguzi wa makosa makubwa, na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao Machi 27, 2026 katika Kijiji cha Mtyangimbole, Kata ya Mtyangimbole, Halmashauri ya Madaba, Wilaya ya Songea, walipokuwa wamejificha.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakijihusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu, ikiwemo uvunjaji na wizi wa pikipiki katika Wilaya ya Songea.

Jeshi la Polisi limesema upelelezi wa tukio hilo unaendelea, na utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

 

Leave a Comment