
Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa nchi yake ina uwezo wa kufungua tena njia muhimu ya mafuta ya kimataifa, Strait of Hormuz, iwapo itapata muda zaidi.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump alisema: “Kwa muda kidogo zaidi, tunaweza kwa urahisi kufungua Hormuz, kuchukua mafuta na kutengeneza utajiri mkubwa.”
Kauli hiyo inakuja wakati presha ikiongezeka kwa utawala wake kutafuta suluhisho la haraka kwa vita vinavyoendelea dhidi ya Iran, ambavyo sasa vimeingia takriban wiki tano tangu kuanza kwake kufuatia mashambulizi ya anga ya pamoja kati ya Marekani na Israel.
Katika hatua ya kulipiza kisasi, Iran imefanikiwa kufunga njia ya Strait of Hormuz, ambayo hupitisha takribani asilimia 20 ya mafuta yote yanayotumika duniani. Kufungwa kwa njia hiyo kumesababisha misukosuko kwenye masoko ya fedha na kupandisha bei za nishati duniani.
