Rais Samia Apokea Ripoti Ya Tume Ya Kuchunguza Matukio Ya Uvunjifu Wa Amani – Video
Global Publishers April 23, 2026 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025, kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Aprili, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, akipokea Ripoti ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Yaliyotokea Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025, tarehe 23 Aprili, 2026, Dar es Salaam
Tume hiyo ilipewa jukumu la kuchunguza matukio ya vurugu, migogoro na uvunjifu wa amani yaliyoripotiwa wakati na baada ya uchaguzi, pamoja na kubaini chanzo chake na kutoa mapendekezo ya muda mfupi na mrefu ya kuimarisha utulivu wa taifa.
Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman akisoma Muhtasari wa Ripoti ya Tume hiyo, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 23, Aprili, 2026. Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya kupokea Ripoti ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Aprili, 2026. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla ya kupokea Ripoti ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Aprili, 2026.