×

Trump Atoa Amri Kwa Jeshi la Wanamaji Kushambulia Boti Zinazoweka Mabomu Hormuz

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa amri kali kwa Jeshi la Wanamaji la Marekani kushambulia na kuua bila kusita boti zozote ndogo zinazodaiwa kuweka mabomu ya baharini katika Strait of Hormuz.

Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa Truth Social, Trump amesema ameagiza operesheni za kijeshi kuimarishwa ili kuondoa mabomu yaliyokwisha wekwa na kuongeza juhudi za kusafisha njia hiyo muhimu ya biashara ya kimataifa.

Amesema pia vitengo vya kusafisha mabomu vya jeshi (mine sweepers) vimeanza kazi kazi kwa kiwango cha juu zaidi mara tatu ili kuhakikisha usalama wa njia hiyo ya bahari.

Hatua hiyo inakuja wakati mvutano ukiendelea kati ya Marekani na Iran, huku hofu ikiongezeka kuwa Strait of Hormuz inaweza kuzuiwa kabisa, jambo ambalo lingeathiri usafirishaji wa mafuta duniani.

Leave a Comment