
Dar es Salaam, Tarehe 23 April 2026: Kampuni ya SanlamAllianz Life Insurance (Tanzania) Limited imezindua rasmi Salama Plan, mpango mpya wa mafao unaolenga kuwasaidia Watanzania wanaokaribia au waliokwisha kustaafu kupata kipato cha uhakika kwa maisha yao yote, pamoja na usalama wa kifedha wa muda mrefu.
Uzinduzi wa mpango huo, umefanyika katika hafla maalum jijini Dar es salaam na kujikita katika kujibu hitaji kubwa na linaoongezeka kwa wastaafu wengi la kuwa na kipato cha uhakika na cha muda mrefu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mtendaji Mkuu wa SanlamAllianz Tanzania, Julius Magabe, alisema:
“Uzeeni unapaswa kuwa muda wa kupumzika, si wa kuwa na wasiwasi. Kupitia ‘Salama Plan’, tunawawezesha watu kufurahia matunda ya kazi zao kwa kujiamini, bila hofu ya kutokuwa na uhakika wa fedha.”
Mpango wa Salama ni suluhisho la kifedha ambalo linakuwezesha mtumiaji kuweka fedha mara moja (one-time premium) nakuweza kupokea pesa yako kila wakati. Wateja wanaweza kuchagua ratiba ya malipo kulingana na mahitaji yao. Kiasi cha chini cha kujiunga na huduma hiyo ni shilingi milioni 5 za Kitanzania, bila kuwa na ukomo wa kiwango cha fedha cha juu, hivyo kufanya bidhaa hii kuwafikia watu wengi zaidi, hususani wale wanaojiandaa kustaafu au waliokwisha kustaafu.
Mbali na kuleta suluhisho la kipato kwa maisha yote ya mstaafu, mpango huu pia unazingatia ustawi wa familia pale mteja anapofariki, kwa kuhakikisha kuwa wanufaika walioteuliwa wanaendelea kupokea malipo kwa kipindi kilichochaguliwa. Aidha, mpango huu pia unatoa nafasi ya dhamana (gurantee periods), vinavyolinda mapato ya mtumiaji wake hata baada ya kifo cha mteja ndani ya muda huo.
Bidhaa hii inalenga zaidi watu wenye umri kati ya miaka 50 hadi 70, wakiwemo wastaafu kutoka sekta ya umma na binafsi, wajasiriamali waliolenga kupunguza shughuli zao za kiuchumi, pamoja na watu wasiokuwa na mifumo rasmi ya pensheni lakini waliokusanya akiba au mali kwa muda.
Akisisitiza umuhimu wa bidhaa hiyo, Magabe aliongeza:
“Tunaelewa changamoto zinazowakabili wastaafu wengi, ikiwemo jukumu la kusaidia familia pana na kupanda kwa gharama za maisha. ‘Salama Plan’ ni namna yetu ya kuwaambia mmefanya wajibu wenu, sasa ni wakati wa kufurahia hatua inayofuata ya maisha.”
Uzinduzi wa bidhaa hii unaashiria mwelekeo mpya kwa Watanzania katika kujiandaa na maisha baada ya ajira, huku ukitoa uhakika wa kwamba urithi wao utaendelea kulinda familia zao. Hafla hiyo pia ilihusisha mijadala ya kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa pensheni, viongozi wa jamii na washauri wa kifedha, jambo lililoimarisha nafasi ya Sanlam Allianz kama mshirika anayeaminika katika mipango ya kustaafu nchini.
Kuhusu SanlamAllianz Tanzania
SanlamAllianz Tanzania ni kampuni inayoongoza nchini Tanzania katika kutoa huduma za bima ya maisha, bima za mali na huduma ya uwekezaji. Sanlam Allianz Tanzania inaundwa na taasisi tatu zinazoongoza sokoni, ambazo ni Sanlam Allianz Life, Sanlam Allianz General, na Sanlam Allianz Investments zikiwa na jumla ya uzoefu wa zaidi ya miaka 50 katika kuhudumia soko la Tanzania. Kampuni hizi zinatoa huduma za bima za maisha , bima za mali na huduma ya uwekezaji. Huduma hizi zinatoa ulinzi wa kiuchumi, uwekaji wa akiba na ulinzi wa bima kwa familia, biashara na taasisi mbalimbali.