×

Trump Amtimua Waziri wa Jeshi la Wanamaji, Marekani Yabadilisha Mkakati Dhidi ya Iran

Aliyekuwa Waziri wa Jeshi la Wanamaji, John Phelan

Mvutano wa kijeshi katika eneo la Strait of Hormuz umechukua mwelekeo mpya baada ya Donald Trump kumfuta kazi Waziri wa Jeshi la Wanamaji, John Phelan, katikati ya operesheni ya kuizuia Iran.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Pentagon, Phelan ameondolewa madarakani mara moja bila sababu rasmi kutolewa, na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Naibu wake, Hung Cao.

Phelan alikuwa na jukumu kubwa katika kusimamia operesheni za kijeshi dhidi ya Iran, hususan katika kudhibiti shughuli za usafirishaji ndani ya mlango huo muhimu wa bahari unaosafirisha sehemu kubwa ya mafuta ya dunia.

Uteuzi wa Hung Cao unakuja wakati hali ya usalama ikiendelea kuwa tete, huku ripoti zikieleza kuwa Iran kushambulia meli kadhaa za mizigo katika eneo hilo, hatua inayozidi kuongeza hatari ya mgogoro mkubwa zaidi.

Akimpongeza mrithi huyo mpya, Trump alimwelezea Cao kama mfano wa ndoto ya Marekani, akitilia mkazo historia yake kama mkimbizi aliyepanda hadi kuwa kiongozi wa kijeshi.

Hatua ya mabadiliko hayo ya ghafla imezua mjadala mkubwa, hasa ikizingatiwa kuwa inakuja wakati operesheni za kijeshi zikiendelea na mazungumzo ya kidiplomasia kati ya Washington na Tehran yakiwa yamekwama.

Wachambuzi wa siasa za kimataifa wanaona hatua hiyo kama ishara ya mabadiliko ya mkakati wa kijeshi wa Marekani, huku mvutano katika eneo la Ghuba ukiendelea kuathiri usalama wa biashara ya kimataifa na usafirishaji wa nishati.

Leave a Comment