×

Mahakama ya Afrika Kusini Yaamuru Mwili wa Edgar Lungu Urejeshwe

Rais wa zamani Edgar Lungu enzi za uhai wake.

Mahakama Kuu ya Afrika Kusini imetoa uamuzi wa dharura ikiitaka Serikali ya Zambia kurejesha mwili wa Rais wa zamani Edgar Lungu, hatua inayokuja saa chache baada ya serikali kudai kuwa tayari imeuchukua rasmi mwili huo.

Kwa mujibu wa uamuzi huo, mwili wa kiongozi huyo wa zamani unapaswa kurejeshwa hadi kesi hiyo itakaposikilizwa tena mahakamani ifikapo Mei 21, 2026. Hatua hii imezidi kuongeza sintofahamu na mvutano katika mgogoro unaoendelea kati ya serikali na familia ya marehemu.

Serikali ya Zambia imeeleza kuwa ilichukua hatua ya kuuchukua mwili huo baada ya kudai kuwa familia imeshindwa kuendelea na mchakato wa rufaa. Hata hivyo, familia kupitia msemaji wake imepinga vikali madai hayo, ikisisitiza kuwa imefuata kikamilifu taratibu zote za kisheria katika kushughulikia suala hilo.

Mvutano huo pia unachochewa na historia ya uhusiano usioridhisha kati ya Edgar Lungu na mrithi wake, Hakainde Hichilema. Familia ya marehemu inaendelea kusisitiza kuwa Lungu hakutaka mazishi yake yahusishe serikali wala viongozi wa sasa, jambo linaloendelea kuwa chanzo kikuu cha mgogoro huo.

Leave a Comment