
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Ndugu Dorothy Semu, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Ndugu John Heche.
Katika kikao hicho, Semu alitembelea Makao Makuu ya CHADEMA kwa lengo la kutoa salamu za mshikamano kufuatia chama hicho kuruhusiwa kurejea katika shughuli za kisiasa baada ya kipindi cha zuio la muda mrefu. Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano na mshikamano miongoni mwa vyama vya siasa nchini.